21 Desemba 2014 - 19:05
Wanajeshi wa Kikurdi Iraq wazidi kusonga mbele

Wanajeshi wa Kikurdi leo wameendelea kuingia ndani ya mji wa Sinjar wakati wakilenga kuukomboa mji huo kikamilifu kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.

Wanajeshi wa Kikurdi leo wameendelea kuingia ndani ya mji wa Sinjar wakati wakilenga kuukomboa mji huo  kikamilifu  kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh.

Wapiganaji wa kikurd almmarufu kama Peshmaege wamefanya mashambilizi makali, sanjari na mashambulizi ya anga yanayoongozwa na Marekani na kuweza kuwa ondoa magaidi wa Daesh katika eneo kubwa la mlima Sinjar iliyoko kaskazin mwa Iraq ambapo magaidi hao waliweka kambi kwa muda mrefu.

Alhamisi ilyiopita, wanajeshi wa Kikurdi walifaulu kuwarudisha nyuma magaidi wa Daesh waliokuwa wameuzingira mlima Sinjar kwa miezi kadhaa, na kuwakomboa maelfu ya raia waliokuwa wametekwa katika sehemu hiyo tangu mwezi Agosti mwaka huu.

Kikundi cha kigaidi cha Daesh kimeripotiwa kuua askari wake wengine thelathini waliokuwa wanataka kukimbia na kujitenga na kundi hilo katili.

Lebo